Baadhi
ya Waandishi wahabari wakifuatilia mkutano huo, Picha
na Hassan Silayo-MAELEZO
Akizungumzia hatua nyingine
zinazoweza kusaidia kuzuia majanga ya moto Mhandisi Majige ni kuepuka kuweka vitu vinavyoweza
kushika moto kirahisi karibu na nyaya ama maungio ya nyaya za umeme ndani ya
nyumba .
Majige alitoa wito kwa watumiaji wa
umeme kutoa taarifa pale wanapotaka kuongeza matumizi ya umeme kwa kiwango
kikubwa ndani ya makazi ya watu ili tathmini ya uwezo wa nyaya kukidhi mahitaji
yaliyoongezeka ifanyike.
Katika kuzuia matukio ya moto TANESCO
imekuwa ikihakisha kuwa inamfikishia mteja umeme ulio salama na usiokuwa na
madhara kwa mtumiaji kutoka kwenye nguzo mpaka kwenye mita.
Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwepo na
matukio ya ajali za moto katika makazi ya watu ambayo yamekuwa yakisababisha
madahara ikiwemo kusababisha
vifo,majeruhi na uharibifu wa mali.
|
Post a Comment