Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia
mkutano huo.
Katika ukaguzi huo ripoti hiyo ilionyesha kuwa
Taasisi hiyo imekuwa ikizingatia sheria na kanuni za matumizi ya fedha za umma
hali iliyopelekea kupata hati safi kwa kipindi chote.
Pia Chuo hicho kilifanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya
Udhibiti wa manunuzi Serikalini (PPRA) kwa mwaka unaoishia 2014/2015 na Chuo
hicho kupata alama 95.8 hivyo kuwa moja ya Taasisi za Umma zinazofanya vizuri
katika kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi ya umma.
Prof. Mjema amesema kuwa chuo hicho kimekuwa
kikijiendesha bila kupata ruzuku toka Serikalini na pia kuzalisha mapato ya
ziada zaidi ya bilioni moja kwa kwa kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka 2013 hadi
2015.
Kutokana na Mafanikio hayo chuo hicho kimeweza
kuanzisha Kampasi ya Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua eneo lenye ukubwa wa
ekari 54.9 na pia maboresho katika maktaba ya chuo yamefanyika.
Mafanikio mengine ni kujenga hema kubwa lenye
uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha karakana ya vipimo na mizani
chuoni hapo.
|
Post a Comment