Header Ads

Tigo yamdhamini BEN POL Kuburudisha Tamasha la Nyama Choma

 Mkuu wa Kitengo cha Burudani na Digitali wa Tigo, Paulina Shao (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tamasha la nyama choma litakalofanyika  Viwanja vya Leaders kesho kutwa Jumamosi Mei 28, 2016 jijini Dar es Salaam, ambapo mwanamuziki Ben Pol atatoa burudani kwa udhamini wa kampuni ya Tigo. Kulia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi na katikati ni mwanamuziki Ben Pol.

 Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.

 Mwanamuziki, Ben Pol (katikati), akizungumza katika mkutano huo.

 Mtaalamu wa Kidigitali, Samira Baamar (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Kampuni inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imekubali kumdhamini mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo za muziki, Bernard Michael Paul Mnyang'anga, maarufu kama ‘Ben Pol’ kuburudisha katika tamasha la mwaka huu la Nyama Choma.

 Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha maarufu linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam litafanyika kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016. 
 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya Dijitali Paulina Shao  alisema kuwa  kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha  kuendelea kujikita kwa Tigo katika  kuwekeza katika kusaidia  sekta ya muziki ya ndani kwa kuhakikisha  wasanii  wanawezeshwa  kufikia viwango vya juu katika kazi zao.

“Kama kampuni ya maisha ya kidijitali, Tigo inatambua  mchango muhimu wa wasanii wa Tanzania  wanaoutoa katika sekta ya burudani. 

Hii ndio maana  tumewekeza kwa kiwango kikubwa  kuwasaidia wasanii  hususani wanamuziki  wa ndani katika kuhakikisha wanafahamika katika masoko ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa kutumia majukwaa ya kidijitali yanayokuwepo na kushiriki  matukio mbalimbali  na hivyo kuongeza  mauzo ya  muziki wao  pamoja na nembo zao,” alisema Shao.

Aidha akiishukuru Tigo kwa uungwaji mkono huo, Ben Pol  aliisifu Tigo kwa juhudi  inazofanya bila kuchoka  katika kukuza  ukuaji wa  sekta ya muziki wa ndani  kupitia Jukwaa la Muziki  la Tigo.

“Ninaishukuru sana Tigo  kwa uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa  programu ambazo imezianzisha  ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa Tanzania,” alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia kuwa wasione aibu  kuomba msaada  kutoka kwa mashirika kama Tigo.

Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava  kwa hivi sasa anatamba na  kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.

Ben Pol ni miongoni mwa wasanii  wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo  ambalo lilianzishwa mwaka 2015 likiwa na lengo la  kuiunga mkono sekta ya muziki Tanzania  kwa kuwasaidia wasanii wa ndani  kupata kipato zaidi kutokana na mauzo ya  kazi zao  na kuwawezesha kufahamika katika masoko ya kimataifa  kupitia majukwaa hayo ya kidijitali  kama vile Music portal na Deezer, ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao yakiwa na  nyimbo kutoka sehemu mbalimbali  duniani  zaidi ya  milioni 36.


No comments

Powered by Blogger.