UONGOZI WA UDSM WAANZA KUWEKA TAA MABIBO HOSTEL.
UONGOZI Chuo Kikuu cha Dar es salam unatarajia kununua taa za dharura 12 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la giza katika Hosteli ya Mabibo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anaeshughulikia masuala ya Utawala Prof.David Alfred Mfinanga wakati wa mahojiano na Idara ya Habari.
Alisema kuwa tatizo la giza nene katika eneo hilo la lango kuu la kuingia Hostel za mabibo mpaka eneo lile la maegesho ya magari lipo mbioni kupatiwa ufumbuzi baada ya taratibu za ununuzi kukamilika.
Alisema kuwa kukamilika kwa uwekaji wa taa hizo za dharura zitapunguza kabisa tatizo hilo.
Aidha, Prof.David Alfred Mfinanga alisema kuwa katika mpango wa muda mrefu wa kutatua tatizo hizo uongozi wa UDSM unatarajia kuweka umeme wa jua ambao utapunguza gharama za kulipia umeme na hivyo kuwa na umeme wa uhakika.
Hostel hizo za kisasa zilizojengwa miaka michache iliyopita na Shirika la Hifadhi za Jamii(NSSF) zimesaidia kupunguza tatizo la makazi lililopo kampasi kuu ya Chuo kikuu(mlimani) lakini kasoro hizi za kukosa umeme zinahatarisha eneo hilo kugeuka kuwa la ubakaji na hata ukabaji kwa wanafunzi na wageni.
Post a Comment