Header Ads

Filamu ya Maisha Kamili ya Wana Vyuo kuingia Mtaani

SERIKALI imeombwa kuunda mbinu mbadala ambayo itaweza kusaidia kuzuia wasanii kuibiwa kazi zao kwa kuweka adhabu kali ambayo itakuwa fundisho kwa wale wanaovunja sheria zilizowekwa kwa mujibu wa bodi ya filamu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa kikundi cha filamu Duse Arts, ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hiko mwaka watatu Kyangala Gosbert, alisema kuwa endapo watafanya hivyo watasaidia kuikuza zaidi tasnia hiyo na kuiingizia nchi sifa ya kuwa na kazi nzuri.

 Mwenyekiti wa kikundi cha Duce Arts na muigizaji katika filamu hiyo, Gosbert Kyangala, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusiana na uzinduzi wa Filamu ya Maisha ya Chuo ambayo itakayozinduliwa juni 3 Mwaka huu katika viwanja vya Chuo vya Duce, Katikati ni Muongozaji wa Filamu hiyo, Manfred Mndanga na Muigizaji, Nyembo Nyembo. Picha zote na Raymond Urio


Alisema lengo ya kusema hayo kundi hilo linatarajia kuzindua filamu yao mpya  iitwayo 'Maisha ya Chuo' inayo tarajiwa kuzinduliwa Juni 3 mwaka huu katika vuwanja vya chuoni hapo wilayani Temeke.
Alisema lengo la kuzindua filamu hiyo ni kutaka kuuelimisha umma na kuwaondolea dhana iliyopo kwenye jamii kuwa maisha ya chuo ni starehe tu siyo kusoma  jambo ambalo siyo kweli.

"Jamii yetu imegubikwa na dhana mbovu kuwa unapokuwa chuo hosteli ubanwi hivyo badala ya kusoma inakuwa ni starehe , hivyo tunataka kuwaelimisha kuwa chuo ni sehemu ya kusoma pia kupitia filamu hii tutawaelisha wanafunzi wenzetu wenye tabia hizo kuachana nazo ili kuweza kutimiza ndoto zao " alisema.


Waigiza na waandaaji wa Filamu Maisha ya Chuo,Kutoka  Kushoto ni Muigizaji wa Filamu hiyo, Rosemary Mbyallu, wa pili kushoto  ni Mwenyekiti wa kikundi cha Duce Arts na muigizaji katika filamu hiyo, Gosbert Kyangala, wa tatu toka kushoto ni Muandaaji wa Filamu hiyo, Manfred Mndanga na Nyembo Nyembo, wakionesha bango la Filamu hiyo amabyo itakayozinduliwa Juni 3 Mwaka huu katika Viwanja vya Chuo cha Duce Temeke Dar es Salaam jana. 

Rese Mary Mbyaru, mmoja kati ya washiriki katika filamu hiyo alisema anawaomba serikali kuwaunga mkono na kuzuia wizi wa kazi zao ili kuweza kufikisha ujumbe stahiki kwa jamii ili kuweza kuondokana na dhana hiyo.

"Filamu hii tumefanya kazi na kampuni ya Bright Star Films Production, ambao wametupa ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha tunafanikisha kazi hii na kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii tukiwa kama walimu watarajiwa wa badae ambao kwa sasa tukiwa bado tupo chuoni tunatumia nafasi hii kuelimisha wenzetu kuachana na vitendo viovu na hatarishi" alisema RoseMary.

No comments

Powered by Blogger.