CHINA yatoa Msaada wa Madawati yenye Thamani ys Shilingi Milioni 20
Wananchi wa kijiji cha Misigili wakiandaa zawadi kwa ajili ya balozi wa China alipotembelea kijiji hicho kutoa msaada wa madawati.
Balozi wa China nchine Dr Lu Yong,ng akifurahia zawadi alizopewa ,kulia ni mbunge Martha Mlata. |
Boga lenye kilo 7 alilopewa balozi wa China Iramba Singida. |
Sehemu ya madawati iliyotolewa na ubalozi wa China wilaya ya Iramba .......................................
SERIKALI ya china imepongeza
jitihada za makusudi zenye mwelekeo wa
kuwsasskomboa watanzania zinazo endelea
kufanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Magufuli kwa kuwa serikali ya mfano ulimwenguni.
Balozi China nchini Tanzania Dr Lu Yong,ng
alitoa pongezi hizo jana katika ofisi za Halmashauri ya Iramba wakati
akikabidhi madawati 400 yenye thamani ya
Tsh milioni 20 kutoka katika ofisi yake na wadau wengine wa maendeleo kikiwemo chama cha wachimbaji wadogo wa
madini nchini ambao waliunga walichangia
madawati 100 kati ya madawati 400 yaliyotolewa na balozi huyo.
Huku balozi huyo akimpongeza
waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba kuwa amekuwa ni
waziri mchapakazi na kiunganishi sahihi kati ya wa wakulima ,wafugaji na wavuvi
kwa serikali na hata nje ya nchi ya Tanzania jambo ambalo limeendelea
kuvutia wengi kuona kuna haja ya kuunga
mkono jitihada za Rais kupitia wizara ya kilimo katika kuwatumikia
wakulima hapa nchini.
Kuwa utendaji kazi wa Rais Dr Magufuli si tu unawavutia wananchi wa Tanzania pekee
bali utendaji kazi wake umekuwa ngunzo na kivutio kwa nchi mbali mbali za
Afrika na hata Duniani kwa ujumla nchi nyingi ikiwemo nchi ya China wamekuwa
wakivutiwa na utendaji kazi wa serikali ya Tanzania chini ya Rais Dr Magufuli.
Alisema kuwa watanzania walifanya maamuzi mazuri katika
uchaguzi mkuu mwaka jana kwa kumchagua mtu sahihi ambae ni Dr Magufuli kuwa
Rais na wananchi wa jimbo la Iramba kufanya maamuzi safi ya kumchagua Bw
Nchemba kuwa mbunge wao na kuteuliwa na Rais kuwa waziri wa wizara nyeti kwa
Taifa ya kilimo.
“Mheshimiwa Mwigulu Nchemba anavyofanya kazi nzuri ya
kuimamia wizara yake bado amekuwa hawasahau wananchi wake wa jimbo la
Iramba katika elimu na kilimo pia jambo
ambalo mimi nampongeza sana nimekuwa
nikifuatilia vyombo vya habari na kuona jinsi
Nchemba anavyojitahidi kupambana na maendeleo ya wananchi wa jimbo lake
pia tutaendelea kuwasaidia maendeleo kupitia kampuni ya China nchini “
Kwani alisema kilimo ni tegemeo kubwa la Taifa hivyo kuteuliwa kwake kuwa waziri wa wizara
hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wakulima na jitihada zake zinaonekana na kuifanya
serikali kuonekana zaidi nje.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na utendaji mzuri na uwajibikaji kwa wananchi serikali ya Rais
Dr Magufuli imeendelea kupongezwa zaidi ulimwenguni.
Aidha alisema kuwa ni
vema kasi iliyopo nchini ya kuwekeza katika sekta ya elimu kuendelea zaidi ili
kupitia elimu kulifanya Taifa la Tanzania
kupaa zaidi katika maendeleo ya
mbali mbali yakiwemo ya Kilimo pia kwani alisema nchini kwake China
sekta ambayo imeheshimika zaidi ni sekta
ya elimu na watumishi wa sekta ya
elimu wakiwemo walimu kwa China ndio
ambao huanza kulipwa mishahara yao kabla ya
sekta nyingine zote.
“ Nchini China walimu
wanapata kwanza mishahara ndipo zinafuata sekta nyingine pia kabla ya
kujenga majengo ya idara nyingine
sisi tumekuwa tukianza
kujenga shule bora ,nyumba
za walimu ndipo tunanza ujenzi wa majengo ya sekta nyingine tumekuwa tukifanya hivyo kwa
kuamini kuwa elimu ni kila kitu”
Kwa upande wake
waziri Nchemba akimpongeza balozi huyo
kwa msaada wa madawati na kuonyesha nia
ya kusaidia wakulima wa Alizeti Iramba kuwa na viwanda vya kuchataka alizeti bado alisema kwa
upande wa wilaya ya Iramba
imekuwa na harambee kubwa ya kuona
upungufu wa madawati 4016 uliopo unafanyiwa kazi kwa nguvu zote .
Waziri Nchemba
alisema tayari wilaya kupitia pesa
za mfuko wa jimbo na harambee ya kuchangia madawati imefanikiwa kupata madawati 10400 ambayo kwa sasa yanaandaliwa na kupitia msaada huo wa madawati kutoka ubalozi wa China nchini jumla ya
madawati ambayo yamekwisha patikana hadi
sasa ni 10800 kati ya madawati
4016 yaliyokuwa yanahitajika .
Hivyo alisema katika kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Singida
juu ya ufumbuzi wa kero ya madawati
Halmashauri ya wilaya ya Singida imejiwekea mkakati wa kumaliza
kero hiyo ya madawati kwa muda mfupi
zaidi ili kuona wanafunzi
wote wanakaa katika madawati
wawapo darasani.
Alisema mbali ya balozi huyo
kufika kukabidhi madawati hayo pia wamelazimika kumpitisha katika tarafa
ya Shelui, Ndago ambako kuna wakulima
zaidi wa kilimo cha Alizeti
kwa lengo la kuwaonyesha
ili waweze kuwashawishi wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza viwanda vya kuchakata Alizeti katika wilaya ya Iramba
.
Waziri Nchemba
alisema iwapo ombi lake kwa ubalozi wa China kuomba
wawekezaji wa viwanda kuja mkoani Singida itasaidia Tanzania ya viwanda kufanikiwa zaidi.
|
Post a Comment