Utalii wa Ndani Waathirika Kutokana na Mwamko Mdogo wa Watanzania
Na. Aron Msigwa - Dodoma
Mwamko mdogo wa Watanzania kutembelea hifadhi za Taifa
zilizo katika maeneo mbalimbali nchini umeathiri kiwango cha idadi ya watu wanaotembelea
hifadhi hizo kwa mwaka hivyo kuzorotesha mapato yanayotokana na watalii wa
ndani ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa
Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe wakati akiwasilisha Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Amesema kuwa licha ya Serikali kuweka gharama ndogo za
viingilio katika hifadhi za Taifa kwa watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki bado mwamko ni mdogo hasa
idadi ya watanzania wanaokwenda kutembele hifadhi hizo jambo linalopunguza
mapato yanayotokana na utalii wa ndani wa watanzania.
Ameeleza kuwa kwa sasa watanzania kwa maana ya watu
wazima wanaotembelea hifadhi za ndani zilizoko eneo la Kaskazini hutakiwa
kulipa kiingilio cha shilingi
elfu kumu (10,000) na shilingi elfu 5000 hadi 15,000 kwa hifadhi zote
zilizoko kusini mwa Tanzania huku watoto wakilipia shilingi 2000 kutembelea
hifadhi yoyote nchini.
Prof. Maghembe ameeleza kuwa kufuatia hali hiyo Wizara
yake inaendelea na kampeni mbalimbali ili kuwahamasisha Watanzania Wengi
zaidi kushiriki katika shughuli za utalii ndani ya nchi hivyo
kuongeza patoa la Taifa.
Amesema katika kulinda na kutunza hifadhi za Taifa ili
kuhakikisha zinakuwa endelevu na kutoa
mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, Serikali ya awamu ya tano imejipanga
kikamilifu ujangili wa wanyama pori kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
uhifadhi.
Amefafanua kuwa katika kupambana na ujangili nchini
Wizara kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi imeshawabaini na kuwashughulikia
baadhi ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi
wanaoshirikiana na watumishi wasio waaminifu kushiriki vitendo vya ujangili pia
kuwashughulikia wawindaji haramu wanaojihusisha moja kwa moja kuua wanyama kufanya udalali na kusafirisha wanyama hao.
Aidha, amesema kuwa katika kupambana na ujangili
Serikali inaendelea kufanya doria ili
kuwashughulikia wawezeshaji ngazi ya nchi wanaonunua nyara, kusambaza silaha,
watakatishaji fedha , majangili nguli wa kimataifa kwa kukitumia na
kukiimarisha kitengo cha Intelijensia ili kiweze kutimiza majukumu ya kiulinzi
kwa ufanisi zaidi.
Pia amesema kuwa Wizara hiyo imeendendelea kuongeza
idadi ya askari wanyamapori 447 na maafisa 111 na kufanya idadi ya watumishi
waliopo kwa sasa kufikia 2,064 pamoja na kuanzisha kada nane za doria za
ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya Selous-Niassa-Mikumi, Ruaha- Ruangwa,
Katavi -Rukwa , Moyowosi -Kigosi, Tarangire- Manyara-Simanjiro na Ngorongoro -
Serengeti.
Post a Comment