Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa
Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake), Menejimenti ya NBS na
wageni walioambatana na Mkurugenzi Mkazi huyo alipotembelea leo, Makao Makuu ya
Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ameishukuru
Benki ya Dunia kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiisaidia Ofisi ya Taifa
ya Takwimu ambayo imeongeza tija katika ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi
nchini.
“Napenda kuchukua
fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kupitia ujio wako kuitembelea Ofisi ya
Taifa ya Takwimu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hii ikiwa
ni pamoja na ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi hapa nchini,” amesema Dkt.
Chuwa.
Dkt. Chuwa amesema
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendelea kupanua wigo wa uzalishaji wa takwimu nchini
ikilinganishwa na karne zilizopita.
Benki ya Dunia
inaisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutoa ushauri wa kitalaam pamoja na
fedha kupitia Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu
nchini ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwezi Juni, 2018.
|
Post a Comment