Wadau mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani
kusaidia Afya (TGPSH) wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu
Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa
Tiba Dkt. Margaret Mbando hayupo pichani
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka
Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
.........
Mbali na hayo Dkt Mbando amesema kuwa amewakaribisha
wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo
yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora”yatayofikia
kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha
yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.
Aidha ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia
ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa
miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.
Kwa upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke
amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania
utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta
hiyo nchini.
|
Post a Comment