Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini Geneva-Uswisi. ..............Mwandishi maalum-Geneva Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.
Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000
Aidha, mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto. |
Post a Comment