Ukistaajabu ya Mussa !!!..Chumba cha Dereva Chaleta Kizaazaa
Sehemu ya tahamani za ndani za Dereva huyo, Feni na Kabati zilizokutwa ndani ya chumba hicho, pamoja na Chupa za plastiki zilizojaa mokojo, nguo zake juu ya chupa hizo.
***************************************
Na Ripota wetu
UKIHADITHIWA na
kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa
amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata
bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa
wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu ulipata
fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya wakazi wa
mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku na
sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo
aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama 'NYATI'.
Akizungumza na mtandao
huu wa Sufianimafoto, Mama mwenye nyumba kuhusu tukio hilo, alisema kuwa siku
ya Mei 23, akiwa ameketi uwanji karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo huku
akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma kutoka
chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu mwaka 2008 na
kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho kupitia chini ya mlango.
********************************************
Kesho yake Mei 24
Baada ya kuona wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita jirani yake
na kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa na mashaka
na chumba hicho.
Mei 25 Mama mwenye
nyumba aliamua kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili Makoye, kutoa taarifa juu
ya wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na kuongozana na Viongozi wengine,
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine Abdalla Mlaliya na Matrida Paston,
waliofika na kujionea hali halisi ya chumba hicho.
Mama Mwenye nyumba, akifungua mlango wa chumba cha mpangaji wake huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakishuhudia.
***********************************
Baada ya viongozi hao
kufika eneola tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo
cha Polisi. Mama huyo alitekeleza
agizo na kwenda kuripoti Kituo cha Mbezi Garden na kuongozana na Mkuu wa Kituo
hicho na baadhi ya askari hadi nyumbani na kukuta hali hiyo ya sintofahamu.
Mama mwenye nyumba,akionesha uchafu uliokutwa chumbani humo.
****************************************
Walipofika eneo la
tukio na kushuhudia hali hiyo, Mkuu wa Kituo aliamuru mlango huo uvunjwe huku
wanachi na Viongozi wa Mtaa huo wakishuhudia na kuingia ndani ambako walikuta
Chumba kizima kikiwa kimejaa Chupa za Plastiki zilizojaa mikojo, Mifuko ya
Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja iliyochomekwa kwenye Soketi ya Umeme ukutani,
Pakiti nyingi tupu za Sigara aina ya Embassy na Kondomu zilizotumika na
zisizotumika.
Mashuhuda wakiwa nje ya nyumba hiyo wakati wa zoezi hilo la kufungua chumba hicho.
*********************************
Baada ya zoezi hilo,
Mwenyenyumba alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka kurejea nyumbani, lakini
Dereva huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa mbali maeneo ya Kunduchi na
kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.
Hadi Mtandao huu
unaondoka eneo la tukio majira ya saa tano usiku bado wakazi wa maeneo hayo
walikuwa wamejazana nje ya Chumba hicho wakiendelea kumsubiri arudi ili kupata
ukweli kuhusu mambo waliyoyaona katika chumba chake.
Baadhi ya majiraji wakiangalia Albam la Dereva huyo,lililokutwa chumbani humo.
***********************************
Aidha Mama mwenye
nyumba aliuambia mtandao huu kuwa mpangaji wake huyo, tangu alipohamia katika
nyumba hiyo mwaka 2008, hakuwahi kumuona akiingia na mwanamke katika chumba
hicho, wala kumuona mgeni wa aina yeyote kwa Dereva huyo,jambo lililomshangaza
kukuta Kondom zilizotumika katika chumba hicho. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa
utayaona ya Firaun.
Majirani wakipekua begi lililokutwa katika chumba hicho.
*******************************
Hadi leo hii Mei 27,
mtandao huu umeshindwa kumpata dereva huyo baada ya kutompata hewani simu yake
ikiwa imezimwa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Leo hii Mei 27, Mama
mwenye nyumba ameripoti kuwa mpangaji wake huyo,hajatokea nyumbani hapo tangu
kutokea kwa tukio hilo ambapo leo, amechukua uamuzi wakuwalipa vijana wa mtaa
huo ili wasafishe chumba hicho.
Tayari tumewalipa pesa
vijana kiasi cha sh.200,000/= ili wafanya usafi na wameshamaliza na kwenda kufukia
bonde la mto Mbezi.
Mashuhuda wakiwa nje ya nyumba hiyo.
Mjumbe Abdallah Mlali (kushoto) akiwa na mama mwenye nyumba na majirani wakionesha uchafu huo.
Mjumbe wa Mtaa huo, Badili Makoye (wa pili kulia) akiwa na Mama mwenye nyumba na baadhi ya majirani.
Pakiti za sigara zikionekana baada ya kukunja godoro.
CHUMBA CHA DEREVA TAX, KWELI BALAAAAAAA
Post a Comment