Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali imeanza
kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) katika kutangaza nafasi
za kazi,kupokea maombi,kuwaita waombaji kazi kwenye usaili na kuwawezesha kutumia
teknolojia hiyo kupata ajira.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam
na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti
ya Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga
kueleza mikakati ya Serikali kuboresha mfumo wa kupokea maombi ya ajira na kuyashughulikia.
“Sekretarieti ya Ajira inatoa rai kwa waombaji
fursa za Ajira kujisajili katika mfumo wa Ajira unaopatikana kupitia anuani ya tovuti
ya www.ajira.go.tz na mfumo wa” job alert system” au kupitia simu za
kiganjani kwa kupiga *152*00# ili
kuomba fursa za ajira zinazopatikana” Alisisitiza Riziki.
|
Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Bi.
Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jijini Dar es
salaam kuhusu utaratibu mpya wa kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
katika kutangaza nafasi za kazi,kupokea maombi,kuwaita kwenye usaili waombaji
wa kazi na kuwapa taarifa za kazi na
kuwawezesha waombaji kupata ajira kwa kutumia mfumo huo (TEHAMA).Kulia ni Kaimu
Naibu Katibu wa Sekretarieti hiyo anayeshughulikia TEHAMA Bi. Mtage Ugullum.
|
|
Baadhi ya
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira uliofanyika leo jijini
Dar es salaam Ukilenga kutoa taarifa kuhusu matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
katika kuendesha mchakato wa ajira katika utumishi wa umma.
............
Akifafanua
kuhusu faida za kutumia TEHAMA kuendesha mchakato wa ajira, Riziki amesema kuwa
mfumo huo unasaidia kupunguza idadi ya siku za kuendesha mchakato wa ajira
kutoka siku 90 hadi 52 kwa sasa.
Aliongeza faida
nyingine kuwa ni Serikali inapanua wigo wa utoaji taarifa za uwepo wa fursa za
Ajira hasa kwa waombaji wa ajira waishio vijijini.
Alisema mfumo
huu unalenga kupunguza changamoto kadhaa zikiwemo malalamiko ya baadhi ya
waombaji fursa za ajira kuhusu upotevu wa maombi yao ya kazi.
Hadi kufikia
Mei, 2016 jumla ya waombaji wa fursa za Ajira waliokuwa wamejiandikisha kwenye
mfumo wa utumaji maombi ya kazi walikuwa (97,765).
Aidha jumla
ya waombaji wa fursa za Ajira 89,484 wamejiunga kwenye mfumo wa kupata taarifa
za uwepo wa fursa za Ajira kupitia simu za kiganjani.
|
Post a Comment