Header Ads

Tafrija Mchapalo wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya Serengeti Premium Lager yafana


Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akitoa hotuba ya  ufunguzi kwa wageni waliohudhuria tafrija mchapalo ya maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996, Pia kulizinduliwa chapa mpya ya Bia hiyo  .hafla hiyo ilifanyika siku ya alhamisi  katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Mgeni Rasmi Waziri Wa Viwanda, Biashara  Na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage (Mb) akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria hafla ya kutimiza miaka 20 ya bia ya Serengeti premium lager .Hafla ilifanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya SBL Nehemiah Mchechu akitoa hotuba yake katika hafla ya kutimiza miaka 20 ya Bia ya Serengeti Premium Lager na pia kuzinduliwa kwa muonekano mupyaa wa bia hiyo mapema siku ya alhamisi.

Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifurahia jambo.

Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie (katikati) akijadiliana jambo na Mkurungezi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyacha na Mkurungezi wa Masoko wa SBL Ceasar Mloka katka tafrija mchapalo ya kutimiza miaka 20 ya bia ya Serengeti Premium Lager. 

Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi akitoa ufafanuzi wa safari ya bia ya serengeti premium lager toka ilipoanzishwa miaka 20 iliyopita ikiwa ni ubunifu wa mtanzania Winston Kagusa. 

Burudani maridadi ikiendelea wakati wa tafrija hiyo.

Mgeni Rasmi Waziri Wa Viwanda, Biashara  Na Uwekezaji, Mh. Chrles Mwijage (Mb) (wa kwanza kushoto )akifurahia muonekano mpya wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya uzinduizi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SBL Nehemiah Mchechu (katikati ) na  Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Baadh ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakiifuatilia kwa makini uzinduizi wa muoenkano mupyaa wa Serengeti Premium Lager. 

Wadau wakipozi katika picha ya chui ambayo ni nembo ya bia ya serengeti.

No comments

Powered by Blogger.