Makamu wa Rais SAMIA SULUHU azungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Finland
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe.
Vesa Viitaniem (kushoto) masuala mbali mbali ya uwekezaji,elimu na uwezeshaji Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe.
Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji
kutoka nchi ya Finland kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati
katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa
viwanda.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam
alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini
Finland Vesa Viitaniem.
Makamu wa
Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha taifa
linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji
wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi
kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda
vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Makamu wa
Rais pia ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Tanzania
katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na kuwezesha makundi mbalimbali ya
kijamii hapa nchini ikiwemo ya wanawake,yatima na vijana.
Makamu wa
Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu
ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na
barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote
nchini.
Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania
nchini Finland Vesa Viitaniem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya
Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa
huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya
kazi zao kwa ufanisi.
Mahusiano
mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi
nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.
Balozi wa
Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem aliongozana na Mke wa Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
Post a Comment