Wataalam Tanzania na Uganda wajadili Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP)
Wataalam mbalimbali
kutoka Wizara na Taasisi za Serikali za Tanzania
na Uganda zinazohusika na mradi wa
ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga wamekutana
jijini Tanga ili kujadili masuala mbalimbali yatakayopelekea mradi huo
kufanyika kwa ufanisi.
Kikao cha Wataalam
hao kimehusisha pia watendaji kutoka
kampuni zitakazotekeleza ujenzi wa bomba hilo ambazo ni Total E&P ya Ufaransa, Tullow
Oil ya Uingereza, na CNOOC ya China.
Kikao hicho cha
Wataalam kitafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara zinazosimamia Sekta
ya Nishati kutoka nchi Uganda na Tanzania
na baadaye Kikao cha Tatu cha Mawaziri wanaosimamia Sekta husika kutoka nchi hizo.
Bomba hilo litakuwa
na urefu wa kilomita 1443 na nchini Tanzania litapita katika mikoa ya Kagera,
Geita, Tabora, Shinyanga, Dodoma, na Tanga.
Mradi huo
utagharimu Dola za Marekani Bilioni 3.5
ambapo bomba hilo litasafirisha mapipa 200,000 kwa siku.
Post a Comment