Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau
mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi
wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016
Jijjini Dar es Salaam.
Na
Beatrice Lyimo, MAELEZO
SERIKALI imeitaka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini
(CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda
vidogo vilivyopo nchini.
Hayo yamesemwa leo
Jijini na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati
wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.
Dkt Mwijage alisema
kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na
Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana
na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.
Alisema katika
kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake
imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo
vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua
uchumi wa nchi.
“Asilimia 25- 40 ya
mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika
kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili
kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema
Mwijage.
Aidha, Dkt Mwijage
alisema, sekta ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi nchini
ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini kuanzia
Novemba 2015 hadi octoba, 2016.
Katika hatua hiyo Dkt
Mwijage alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza
katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu la
Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na inajenga mazingira wezeshi
kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya biashara.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo
yanaonyesha mafanikio katika sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa ajira
zipatazo 264,223 nchini na kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi bilioni 8.0
kwa mwaka 2013.
Alisema kuwa Takwimu
za matokeo ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka watunga sera,
wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu binafsi kutumia matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya
viwanda nchini.
|
Post a Comment