Mkuu wa Wilaya ya MUHEZA akagua Ujenzi wa Zahanati ya Kijini cha ZENETI
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat
Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya
Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti
wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa
ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na
Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni
35.2.
Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,
Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona
jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto kwake ni Mwenyekiti wa
Serikali ya Kijiji cha Zeneti.
Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat,
Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiingia kwenye vyumba vya zahanati mpya
ya Zeneti kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Lwiza
Mlelwa.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya
Muheza,Mathew Mganga kulia akisisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya
Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kushoto kuhusu
ujenzi wa zahanati hiyo katikati ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid
Mdachi.
Diwani wa Kata ya
Potwe,Rashid Mdachi akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat
Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia.
Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akizungumza na wananchi katika ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya katika Zahanati ya Kijiji cha Zeneti. |
Post a Comment