Makamu wa Rais SAMIA SULUHU afungua Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah Hall,tayari kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe walihudhuria mkutano wakimsikiliza Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikikata utepe kuashiria kuzindia kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiongoza viongozi wengine kuonyesha juu kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kuashiria kimezinduliwa rasmi kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
..............................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku
uharibifu mkubwa wa mazingira unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambao
unaweza kusababisha nchi kugeuka jangwa.
Makamu wa
Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira
chini ya Usimamizi wa Kigoda cha
mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais ameonya kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke yake bali
ni kila mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo wananchi ni muhimu
kwa umoja wao wakaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yao ili
kukabiliana na hali tete ya uhabifu wa mazingira nchini.
“Uharibifu wa mazingira usimame leo na marekebisho
ya uharibifu tulioufanya uanze leo na hili ni jukumu la kila Mtanzania” Makamu wa
Rais pia ametoa wito maalum kwa viongozi wa ngazi zote nchini kuchukua hatua
katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yao ili visitoweke.
Makamu wa
Rais ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza kuleta athari si
kwa Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili
kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa zinakabiliwa ipasavyo.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya Tabia ya nchi,Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Pius Yanda amesema mkutano huo wa siku TANO
utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Post a Comment