Mbunge VENANCE MWAMOTO akabidhi Vifaa vya Michezo Katika Jimbo la Kilolo
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo.
Mbunge
wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa
mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa
mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji
wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa
na mbunge wa jimbo la kilolo.
Mbunge
wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa
mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa
mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji
wa timu ya wanawake wa kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa
na mbunge wa jimbo la kilolo.
Mbunge
wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa
mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa
mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji
wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa
na mbunge wa jimbo la kilolo.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance
Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na
timu za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza
vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.
Mwamoto ametekeleza ahadi
hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika
ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa
kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa
vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao
kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao
pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.
“Niliahidi kuleta vifaa vya
Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan
leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto.
Mwamoto ameongeza kwa kusema
ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua
michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
“Mimi nimecheza mpira kwa
mafanikio ndio maana hadi saizi,kwa hilo mimi najua kuwa michezo ni ajira rasmi
hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”. Mwamoto.
Amesema kuwa michezo licha
ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana
Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo
ikiwemo seti nzima za Jezi na mipira ya
kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao
wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
“Leo nimetoa mipira na jezi
hizi kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya jirani kwa timu zote za wanaume na
wanawake kwa lengo la kuendeleza vipaji vyenu”alisema Mwamoto.
Aidha, amewataka Vijana hao
kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya
vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa
miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana
walio pembezoni.
Post a Comment