Vijana Watakiwa Kuacha Kila Mara Kuihoji Serikali na Badala Wajikite Kufanya Kazi
Kufuatia changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam kuelekea sherehe za maadhimisho ya wiki ya Umoja Mataifa, amesema vijana inabidi wawajibike katika kuleta maendeleo ya uchumi kwenye jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.
Pia amesema vijana waache kuhoji serikali kuwa inawafanyia nini badala yake wawe wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Taifa lao.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
"Tuna kazi kubwa ya kujenga fikra za vijana kwamba ili kufanikiwa katika maisha siyo lazima kuajiriwa, vijana wengi ukiwahoji wanakwambia changamoto kubwa wanayoikabili ni ukosefu wa ajira. Lakini wanasahau kuwa changamoto zipo nyingi zinazowakabili," amesema.
Prof. Ole Gabriel amezitaja changamoto nne zinazokabili vijana ambazo zinasababisha washindwe kujiajiri au kushindwa kujiendeleza pindi wanapojiajiri kuwa ni, ukosefu wa fikra kutokana kwamba wengi hawaziruhusu fikra zao kubuni mbinu za kujiajiri, Changamoto nyingine aliyoitaja ni vijana kukosa uelewa, mbinu na ubunifu wa kuongeza thamani ya shughuli wanazofanya.
Changamoto nyingine aliyoitaja ni mfumo mbovu na usio rafiki kwa vijana hasa mifumo duni ya upatikanaji mitaji na masoko, hususani katika kipindi hiki ambacho kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.
Ameshauri kuwa "Hivi sasa kuna elimu ya ujasiriamali lakini niseme tu haitomsaidia kijana kujikwamua sababu hutoa elimu ya uzalishaji pekee. Ili kijana afanikiwe na ujasiriamali, kwanza inabidi apewe elimu ya kufanya utafiti wa bidhaa inayohitajika kwa kipindi husika, akishajua bidhaa hitajika ndipo afanye uzalishaji kisha hatua ya mwisho kutafuta masoko ambayo tayari ameshayafanyia uchunguzi."
Pia ameshauri vijana kuwekeza katika biashara kilimo kwa kuwa ndiyo sekta pekee yenye fursa ya kutoa ajira kwa wingi kwa kuwa imeajiri asilimia 84 ya vijana.
"Tanzania ina vijana zaidi ya milioni 16.2 ni sawa na asilimia 70 ya watanzania, waliofanikiwa kuajiriwa katika sekta binafsi ni milioni 1, waliojiajiri milioni 1.1 waliopo katika sekta ya umma ni 18,8000 na katika sekta ya kilimo wapo vijana milioni 13.2 na bado nafasi zipo katika sekta hiyo," amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza machache kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Hata hivyo, Prof. Gabriel amewaasa vijana kutotumia utandawazi vibaya hasa mitandao ya kijamii kutokana kwamba imekuwa sababu ya vijana wengi kutokuwa na maadili.
"Utandawazi unabomoa uwezo wenu wa kufikiri, zamani vijana walikuwa wanakimbilia kuwekeza katika sekta ya kilimo ila sasa kutokana na utandawazi wanakimbilia kutafuta ajira hata kama fursa hakuna," amesema na kuongeza.
"Msipoangalia miaka michache ijayo tutakuwa watu wa teknolojia na mitandao. Maadili mema tuliyojengewa yatapotea kwa sababu ya kufikiri kwamba mitindo ya kimaisha kutoka nje ndiyo inafaa kuliko ya kwetu, inabidi turudishe yale maadili ya zamani sababu nchi yoyote isiyokuwa na maadili, tamaduni imeparanganyika na haina maendeleo," amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza kwa niaba ya UN amesema kuwa shirika hilo litahakikisha linawezesha vijana kushiriki katika maendeleo ya uchumi kwa kuwainua kiuchumi pamoja na kutoa elimu ya namna ya kujiajiri.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza jambo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mbunifu wa mavazi Johari Sadiq akizungumzia jitihada, changamoto, fursa na mafanikio aliyoyapata katika yake ajira binafsi kama mtoto wa kike, kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
MC maarufu nchini ambaye pia ni Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda akizungumzia ajira yake binafsi na mafanikio aliyonayo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji ambaye ni Mjasiriamali kijana Stella Imma, akizungumza kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa tatu kulia) akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Post a Comment