Siku ya Watoto wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi yaadhimishwa Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi akifungua rasmi sherehe za kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto takribani 202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima.
Mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Bw. Hakim ambaye nae mtoto wake anamatatizo kama hayo akielezea kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa kuwa watu wengi wanahusisha tatizo hilo na imani potofu, aliongeza kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji mkoa wa Mbeya ni 18, Morogoro 12, Mwanza 50, na Izazi 14. na wamefanikiwa kuokoa Maisha ya watoto 185 katika mikoa 16 Tanzania.
Meneja wa Nakiete akitoa neno wakati wa Maadhimisho hayo.
Mmoja wa wazazi akiwa na Mwanae mwenye tatizo la Kichwa kikubwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi (Kushoto) akipokea Msaada kutoka Duka la madawa la Nakiete.
Madam Sophia Mbeyela (Kulia) akitoa msaada kwa watoto hao.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao wenye vichwa vikubwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi wapili kutoka kushoto akipokea Msaada viti 15 vya kutembelea 'wheel chair' watoto kutoka kwa Mohamed Punjan Foundation.
Baadhi ya wauguzi wakiwa katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wazazi na walezi na wazazi wenye kichwa kikubwa na Mgongo wazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
Picha zote na Fredy Njeje
Post a Comment