Baadhi ya washiriki wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi
wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC)
Prof. Innocent Ngalinda wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika leo
katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.
Na Albert Fen
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika(EASTC) Prof.
Innocent Ngalinda amezindua mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi ambayo
yalianza tarehe 17 Oktoba mwaka huu chuoni Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Prof. Ngalinda
amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa
nia ya kumpatia mshiriki ujuzi katika ukusanyaji takwimu kwa ajili ya
kuzichakata na kuwa takwimu rasmi.
“Washiriki hawa watafundishwa mbinu shirikishi, utatuzi wa matatizo
mbalimbali wakati wa ukusanyaji takwimu, sensa na viwango vya tafiti mbalimbali,
utunzaji wa Vifaa vya ukusanyaji takwimu kama vile simu za mkononi na kumpyuta mpakato pamoja na kubadilisha
madodoso ya kawaida na kuwa ya kisasa”, amesema Prof. Ngalinda.
Akizungumzia malengo ya mafunzo hayo Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti
na Ushauri wa Kitaalamu wa chuoni hapo Dkt. Frank Mkumbo amesema lengo ni
kuwawezesha wakusanyaji takwimu kukusanya takwimu halisi na zenye ubora kwa
ajili ya kupanga mipango mbalimbali ya Maendeleo.
“Lengokuu la mafunzo haya
ni kuhakikisha kuwa wakusanyaji takwimu rasmi wanakuwa na weledi wa kutosha katika kukusanya
takwimu bora na zenye tija kwa taifa” amefafanuaDkt. Mkumbo.
Jumla ya washiriki 110
wamejiunga na mafunzo hayo maalumu ya muda wa miezi miwili kwa awamu ya kwanza ambayo yatamalizika mwezi Disemba,
2016 na watakaomaliza na kufaulu watapatiwa cheti cha Ukusanyaji Takwimu. Awamu
ya pili ya mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu na kumalizika Januari,
2017.
|
Post a Comment