Makamu wa Rais SAMIA SULUHU akutana na Balozi wa India Pamoja na Sudan
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya (kushoto) aliyemtembelea Makamu wa
Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Sudan nchini Mahgoub A. Sharfi (kushoto) alimtembelea na kufanya
mazungumzo na Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
serikali itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati
ya Tanzania na India ambayo yamedumu kwa muda mrefu hasa katika sekta
mbalimbali ikiwemo za elimu,afya na biashara.
Makamu wa
Rais ametoa kauli hiyo leo 25-Okt-2016 wakati alipokutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa India nchini Sandeep Arya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais amesema mahusiano kati ya Tanzania na India yamesaidia kunufaisha wananchi
wa nchini mbili hasa katika masuala ya kibiashara,miradi ya maendeleo na hivyo
mahusiano hayo ni muhimu yakaendelezwa na kudumishwa.
Makamu wa
Rais katika mazungumzo na balozi huyo wa India hapa nchini Sandeep Arya pia
ameiomba serikali kuisaidia Tanzania katika mpango utakaosaidia wakulima kupata
taarifa mbalimbali zinazohusu kilimo na masoko ya bidhaa zao kupitia simu za
mkononi ili kuondoa usumbufu mkubwa wanaopata wakulima kwa sasa hasa kuhusu
masoko.
Kwa
upande wake, Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amemhakikishia Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan serikali
yake itakuwa bega kwa bega na Tanzania katika kuhakikisha wananchi wa pande
Mbili wananufaika na mahusiano yaliyopo.
Balozi
Sandeep Arya amesisitiza kuwa serikali ya India itaendelea kuisaidia Tanzania
katika uimarishaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na miradi ya
maendeleo na uimarishaji wa shughuli za kiuchumi.
Wakati
huo huo, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Sudan nchini Tanzania Mahgoub Sharfi mazungumzo
yaliyolenga pamoja na mambo mengine kuhusu namna ya kuimarisha mahusiano kati
ya Tanzania na Sudan.
Post a Comment