Serikali imesema hakutokuwa
na matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya habari katika
muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa masuala yatakayohatarisha usalama
wa Taifa.
Imesema Serikali
haiwazuii waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali
zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza maagizo
wanayoyatoa kwa wananchi.
Akizungumza katika mwendelezo
wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema muswada
huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake mahakamani
pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa na Waziri mwenye dhamana ya habari.
Kwa mujibu wa Abbasi alisema yapo masuala
kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi ikiwemo suala la uchochezi,
uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka kuigombanisha Serikali na wananchi.
Aliongeza kuwa hata
katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka
1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika
masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.
|
Post a Comment