Kampeni ya Kupiga Vita Ndoa na Mimba za Utotoni ya Binti wa Kitaa yafanyika Tabata
Bibi Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto wao.
Furahini Michael akiulizwa swali na Bwana Steven Mfuko kuhusu athari za mimba za utotoni na kuolewa katika umri mdogo.
Mkazi wa Tabata kwa Cecy ambapo kampeni ya Binti wa kitaa ilifanyika Bi.Sheira Mheni akielezea jinsi watoto hususani wa kike wenye umri kati ya Miaka 12-17 walivyoharibika kutokana na mabadikiko ya Teknolijia ambapo imewapekea kufahamu mambo ya wakubwa wakiwa watoto na hatimaye kupata matamanio na kufanya kama walivyo ona katika Mitandao ya kijamii na Runinga jambo linalowasababishia Mimba za Utotoni.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tenge Athuman Mpwenewe akieleza namna ambavyo kumekuwa na Mimba nyingi za utotoni katika mtaa wake na juhudi ambazo zimefanywa na Serikali ya Mtaa kuhakikisha swala hilo linatokomezwa kabisa na mwisho alizungumzia vikao na wanamtaa vinavyosaidia kutatua tatizo hilo.
Aliyemwakilisha Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata Sajenti Geoffrey Kapenejele ambaye pia yupo katika Dawati akielezea namna wanavyotoa elimu kuhusiana na Jinsia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashuleni pia kwa madereva Bodaboda ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha Mimba nyingi za utotoni, Mwisho aliomba jamii kwa ujumla kushirikiana ili kupiga vita swala hilo.
Bwana nidhamu wa Madereva wa Bodaboda kituo cha Cecy Bwana Atupele akieleza namna elimu ya maswala ya Jinsia ilivyo wasaidia wao kuunga mkono kupambana na mimba za utotoni ambapo wamejiwekea utaratibu wa adhabu kali kwa yeyote atakayempa mimba binti mwenye umri wa chini ya miaka 18.
Mabinti wakiwa katika Kampeni ya Binti wa Kitaa.
Picha zote na Fredy Njeje
Post a Comment