Waziri wa Viwanda CHARLES MWIJAGE azindua Mashine ya Kusaga na Kukoboa Nafaka
“Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage.
Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki.
Alitoa wito kwa mshiriki atakayeshinda Tzshs. Milioni 30 za Maisha Plus aziwekeze katika uchumi wa viwanda.
Grace PEMBA kutoka Mtwara aula
Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane.
"Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho."
GRACE Pemba kutoka MTWARA aula. Waziri Charles Mwijage amemuahidi kumpatia mashine yenye thamani ya shilingi milioni 8 ya kubangua korosho. Mhe. Mwijage ameyasema hayo wakati wa kuzindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka iliyofanyika kijijini @maishaplus #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu A video posted by Masoud Kipanya (@masoudkipanya) on
Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi.
Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter.
Post a Comment