Wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa PWANI wachangia Ujenzi wa Daraja
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wakikagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti. |
...............................................................
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wamefanya Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala lililopo Wilaya Mpya ya Kibiti na kukabidhi kiasi cha milioni moja 1.000.000/= huku shilingi milioni Nne na elfu Hamsini zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti na kufanya jumla ya fedha ya mchango walioutoa katika ujenzi wa daraja hilo kufikia shilingi Milioni Tano na Elfu Hamsini 5.050.000/=.
Msaada huu unafuatia Ahadi iliyotolewa na Wabunge hao wakati wa Kampeni katika kusaidia Wananchi wa Maeneo ya vijiji hivyo ambao kwa sasa wanatumia Daraja la Muda lililojengwa kwa miti na wananchi wenyewe ili kuwawezesha Kuvuka mto .
Ni muda mrefu sasa hawana daraja ambapo kipindi cha mvua Maji hujaa na kuwapa shida wananchi hasa Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi hushindwa Kuvuka na baadhi yao wamepoteza Maisha kwa kusombwa na maji kutokana na tatizo la kukosekana kwa Daraja hilo.
Bajeti ya Ujenzi wa Daraja hilo imefika Milioni Kumi ambapo wabunge hao wamewashukuru Wadau wote waliowaunga Mkono katika kutimiza Ahadi hii ya kusaidia Wananchi wa Vijiji takriban saba hususan Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi ili kuvuka usalama wanapokwenda Kupata huduma mbalimbali zikiwemo Afya na Elimu nk.
Wabunge hao waliwaomba wadau mbalimbali walioahidi kuchangia ujenzi wa daraja hilo katika Kata Mbili za Maparoni na Msala na Wilaya ya Mafia kukamilisha ahadi zao mungu awajaalie wafanikiwe kupata chochote ili waweze kuchangia ili tuweze kukamilisha ujenzi huo ambapo bado unahitaji shilingi milioni 5.000.000 zingine ili kukamilisha bajeti ya ujenzi wa daraja hilo ambayo ni shilingi milioni kumi 10,000.000.
"Tunaamini mtakapo pata fursa Mtachangia Mwenyezi Mungu Awawezeshe Amiin" Alisema Mh. Subila Mgalu huku akimaliza kwa kuwashukuru Viongozi wa Chama, Jumuiya zake , Serikali Ngazi ya Wilaya na Kata kwa mashirikiano makubwa na mapokezi Mazuri .
Daraja litakapokamilika litasaidia Vijiji Saba Kipoka , Usimbe ,Maparoni ,Msala ,Twasalie ,Kihasi ,Kiechuru ,Kibanjo Kata Tatu na pia Njia hii inatumiwa Kufika mpaka Mafia. ambapo kwa sasa kumekuwa na athari yingi hasa kwa akina Mama wengi wajawazito wanashindwa kuvuka Maji yanapojaa na kupelekea kujifungua Njiani.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akifurahia jambo wakati wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu wakionyeshwa vipimo vya daraja na wananchi wakati wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akiwa amekaa na wakina mama wakati wa ziara hiyo wilaya mpya ya Kibiti.
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wakikabidhi fedha taslimu shilingi milioni moja kwa kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti.
Hali ya Vyombo vya Usafiri waliyoikuta wabunge hao wakati walipofanya ziara Mwaka Jana 3/10/2015 ambayo iliwagusa na kuwahamasisha kutafuta Michango ya ujenzi wa daraja hilo Daraja.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
Post a Comment