Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.
..................
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli, leo tarehe 31 Oktoba, 2016 ameondoka
nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini
humo kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali
wa serikali akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam, Paul Makonda na viongozi mbalimbali
wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mara baada ya kuwasili
nchini Kenya, Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru
Kenyatta, na baadae atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa
Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
Mheshimiwa Rais pia
anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini
Nairobi.
Katika ziara hiyo Rais
Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi na pia
kuzindua barabara mchepuko (Southern
By-pass) iliyopo Jijini humo. Barabara hiyo ni moja kati ya miradi mikubwa ya
barabara nchini Kenya, inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara
za juu na chini.
Naibu Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es
Salaam
31Oktoba,
2016
|
Post a Comment