Waziri
wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto mstari
wa Mbele) na Waziri wa Nishati na
Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi
Irene Muloni (wa Pili kushoto mstari wa mbele) wakitoka katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga baada ya kukagua
sehemu itakayojengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada
ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda.
................
Waziri
wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni wametembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga
ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali ili
kusafirishwa.
Mafuta
hayo yatapakiwa kwenye Meli hizo baada ya kusafirishwa na Bomba kutoka Hoima nchini
Uganda kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
Akiwa
katika eneo hilo Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda aliwaeleza
wananchi wa eneo hilo kuwa nchi ya Uganda inaishukuru Tanzania kwa kukubali
Bomba hilo lipite katika ardhi ya Tanzania suala ambalo litakuwa na faida
mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi.
Alisema
kuwa lengo ni kuona kuwa mradi huwa huo
unaanza kazi mwaka 2020 na ndiyo maagizo ambayo Marais wa nchi mbili wameyatoa
kwa watendaji wanaosimamia Mradi huo wa Bomba la Mafuta.
Mhandisi
Muloni alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kujiandaa kikamilifu kwa fursa za
kiuchumi kwani watekelezaji wa mradi watahitaji huduma mbalimbali kama za
chakula, malazi na usafiri hivyo kupitia
utoaji wa huduma hizo wananchi nao watapata kipato.
Pia
alizishukuru Sekta Binafsi za Uganda na Tanzania kwa kuwa tayari kushirikiana
na Serikali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa akitolea mfano kampuni
ya GBP ya Tanzania ambayo imeonesha nia ya kununua hisa katika kampuni
itakayoanzishwa kwa ajili ya usimamizi wa Bomba hilo la Mafuta.
|
Post a Comment