Maonesho ya Bidhaa za PLASTIC, KEMIKALI ZA PETROL na UJENZI kufanyika Jijini Dar es Salaam
Meneja Mkuu wa Expo One, Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni kuhusu maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Hamza Mohamed Hamza akizungumza katika mkutano huo.
Taswira meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Africa-PPB Tanzania, Mohamed Sami akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Khaled Abu El M karem akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Doto Mwaibale
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi yanayotarajiwa kufanyika katika Mei 27 hadi 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Expo One, Ahmed Barakat, alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zitashiriki katika maonesho hayo.
Alisema Maonesho ya Afrika –PPB-EXPRO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya na yatatoa mwanya wa kuyaelewa masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.
“Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha kuwa Tanzania ni ya kwanza katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
“Aramex Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji kutoka Misri hadi Tanzania,” alisema.
Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.
Alieleza kwamba kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza, hii inatoa fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.
Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara.
“Kwa kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri biashara zao, umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.
“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya biashara ya kimataifa pamoja na
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
Alisema kwamba maonesho mengine ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.
Post a Comment