Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Christopher Chusi akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa uliofanyika Mei 30, 2016 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. ......
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele alibainisha umuhimu wa Mpango huo ikiwa ni sehemu ya kuanzia na inayotoa muongozo mzuri unaosaidia katika Halmashauri yake katika kukabiliana na Maafa.
“Tangu mpango kuanza kutumika Desemba 2013 Wilaya ya Kilosa imeweza kuwa na mbinu za kuyakabili maafa yanapotokea hususani yale ya mafuriko” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bw. Idd Mshili aliipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona umuhimu wa kuitembelea Halmashauri yao kwa kuupitia Mpango na kuuboresha ili kusaidia kurahisisha uelewa kwa kua lugha ya Kiswahili inaeleweka kwa urahisi hususani ngazi ya chini na kwa wanavijiji wanaokumbana na maafa pindi yanapotokea.
“Nichukue fursa hii kuwapongeza Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuona umuhimu wa kuubadili mpango kutoka lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili ili kufikia makundi yote ya jamii kwa urahisi.”
AWALI: Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa ulianza kutumika mwaka 2013 ikiwa na lengo la kuziwezesha Halmashauri kujiandaa na kuyakabili maafa yanapotokea, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kufanya Tathimini kwa Halmashauri za baadhi ya Mikoa kwa kuangalia ubora wa mpango tangu uanze kutumika katika Mikoa ya Mtwara, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Singida na Shinyanga kuanzia Mei 23 hadi 30, 2016.
|
Post a Comment