Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Francis Assenga (Kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu matarajio ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo katika kusaidia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw.Thomas Samkyi na kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara Bw. Robert Pascal. ..................
Aidha, Bw. Semkyi alifafanua kuwa mikopo hiyo inalenga kuwanufaisha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa kwa ajili ya kuziba pengo la upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mikopo na Usimamizi wa Biashara wa Benki hiyo Bw. Robert Pascal alisema kuwa kwa miradi mikubwa ya kilimo inayoendeshwa kati ya Serikali, Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi, mikopo ya moja kwa moja itatolewa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya kilimo hasa kuimarisha mifumo ya minyororo ya kuongeza thamani katika mazao ya kilimo.
Pia Bw. Pascal alieleza kuwa Benki hiyo itatumia bidhaa mbalimbali zenye ubunifu katika kuwezesha vikundi vya wakulima wadogo, wafugaji wa ng’ombe, samaki na kuku.
Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) imeanzishwa mwaka 2014 kwa madhumuni ya kutekeleza Sera za Serikali kuhusu upatikanaji wa fedha za kuendeleza kilimo.
|
Post a Comment