MSD " Hali ya Upatikanaji wa Dawa Nchini ni ya Kuridhisha "
.................................................................
Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali
imewahakikishia Watanzania kuwa kuna utoshelevu wa dawa kwa asilimia 86 kinyume
na taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bohari kuu
ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Rugambwa
amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imetenga bajeti yakutosha kukidhi
mahitaji ya dawa hapa nchini ambapo kufikia machi 2017 upatikanaji wa Dawa
utafikia asilimia 90.
“ Serikali imetenga
bilioni 250 katika bajeti ya mwaka huu na Kila mwezi Serikali inatoa zaidi ya
bilioni 20 ajili ya ununuzi wa dawa hali
iliyosaidia kuondoa tataizo la dawa hapa nchini kwa sasa”.
Akifafanua
Rugambwa amesema kwa sasa fedha sio tatizo kwa Bohari ya dawa kutokana na hatua
za makusudi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha
kuwa Watanzania wanapata huduma bora za afya ikiwemo upatikanaji wa dawa.
Moja ya
mikakati iliyochukuliwa na Serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa
dawa ni kuboresha matumizi ya mfumo wa
msimbo pau (Barcode) hali itakayosaidia kuongeza ufanisi katika
upokeaji,utunzaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba.
Mikakati
mingine ni kuanziasha mpango wa huduma maalum kwa wateja wakubwa ambao ni
Hosipitali ya Taifa Muhimbili,MOI, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hospitai
ya Bugando,Hosipitali ya Kibongoto,Hospitali ya Mirembe,Hospitali ya Amani,
Hospitali ya Temeke, Mwanenyemala,Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya,KCMC,
Hosipitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Pia kununua
dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji na kuanzisha mchakoto wa ujenzi wa
viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba nchini ili kupunguza gharama.
Katika
kipindi cha mwaka 2016 MSD imefungua maduka ya dawa sehemu mbalimbali nchini
lengo likiwa ni kuwezesha Hospitali ambazo ndio wateja wakubwa wa MSD,Maduka
ambayo mpaka sasa yameshafunguliwa ni pamoja na lile lililopo katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili,Sekou Toure Mwanza,Hospitali ya rufaa Mbeya,Mount Meru
Hospitali ,Chato Halmashauri ya Mji wa Geita na Ruangwa Mkoani Lindi.

Post a Comment