Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Profesa Ibrahim Gambari ambaye
ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
..................................
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo
na Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria Profesa Ibrahim Gambari nyumbani kwake
Chato Mkoani Geita. Mazungumzo yao yalilenga masuala mbalimbali ya uhusiano
kati ya Tanzania na Nigeria.
Rais Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari
kwa jitihada kubwa anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwaka.
Pia, Rais Magufuli amempongeza Rais Buhari kwa
jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko haramu ili kuhakikisha amani
inaendelea kudumu nchini mwake.
Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Rais wa
Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais Magufuli kwa ushindi
alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na kubana matumizi
jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa Nigeria.
Profesa Gambari alimkabidhi Rais Magufuli barua
yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria.
Jaffar
Haniu
Naibu Mkurugenzi
wa Mawasiliano, IKULU
Chato,
Geita
10 Januari,
2017
|
Post a Comment