Bodi Mpya ya TANAPA yazinduliwa na Waziri JUMANNE MAGHEMBE
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof,Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi
vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Dkt Chanasa Mpelumbe Ngeleja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanika katika ukumbi wa Mhakama ya Afrika jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini iliyomaliza muda wake Modestus Lilungulu walpkutana katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi mpya .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja katika shirika hilo.
Post a Comment