Header Ads

THOBIAS MWILAPWA aingilia Kati Mgogoro wa Wafugaji na Mwekezaji

 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirika na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
..............................


Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameingilia kati mgogoro wa wafugaji na mwekezaji wa shamba la mkonge la Marungu Mkoani Tanga na kutoa miezi mitatu kwa wafugaji hao kuhakikisha wanaondoka katika shamba hilo kabla ya serikali haijatumia nguvu ya kuwahamisha.


Akizungumza katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.


Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lililotolewa siku chache zilizopita na Mh;WAziri MKuu la kuwataka Wakuu wote wa Wilaya nchi nzima kuhakikisha wanamaliza migogoro ya ardhi iliyondani ya uwezo wao ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na shughuli zao.


Mwilapwa alisema kumekuwepo na madhara mengi yanayojiketokeza kutokana na kuwepo kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hadi kufikia kutokea mapigano yanayohatarisha amani iliyopo baina ya makundi hayo mawili jambo ambalo serikali imejidhatiti kumaliza migogoro hiyo kwa makubaliano ya mazungumzo.

 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo.

 Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo.

 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiandika baadhi ya maswali ya wananchi ambao walikuwa wakiuliza kwenye mkutano huo.

 Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu huyo wa wilaya.

No comments

Powered by Blogger.