AU kujiondoa Katika Mahakama ya ICC
Umoja wa Afrika umeunga mkono mpango
wa kujiondoa kwa pamoja katika mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya
Afrika yanahisi inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee.
Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo.
Viongozi
wa Afrika wanasema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa Sudan
Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa
kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
Mpango huo unapendekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha
mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki
za binaadamu.
Post a Comment