Wakulima Nchini Watakiwa Kutumia Teknolojia yenye Tija ili Kupata Mazao yenye Ubora
mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho
ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani.
Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matone.
Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi.
Na Woinde Shizza, Arusha
sekta
ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufugaji holela , ambao hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni
pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo.
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho
ya zana za kilimo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni
mara ya kwanza kufanyika .
Alisema
kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao
unasababishwa na wafugaji ,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika
ukulima pamoja na wakulima wengi kukosa
mitaji ya kubesha miundo mbinu ya kilimo
Alisema
kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii
kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo
cha kisasa ambacho kinaleta tija .
“hapa
Tanzania zaidi ya asilimia 75% wanategemea kilimo lakini kati yao n asilimia
1.5 tu ndio wanatumia kilimo cha kisasa
kama kilimo cha umwagiliaji ,kupanda mbegu
bora pamoja na kilimo cha matone
hivyo ni vizuri wakulima wetu kujitaidi kutumia kilimo cha kisasa ili kuweza
kufanya kilimo chenye tija ambacho kinamnufaisha yeye mkulima mwenyewe na
kuachana na kilimo cha kawaida au naweza sema cha kienyeji”alisema Daqarro.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani
Dr Daniel Mafuru amesema kuwa wamekua
wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo ,katika uzalishaji wa Teknolojia
,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.
Aidha alisema kuwa
Seliani wapo tayari kuwaunganisha
wakulima na waonyeshaji wa teknologi ,ilikuwawezesha wakulima kupata mafunzo na
kubadilishana ujuzi pia iwapo watauwaunganisha
itawasaidia kufahamu namna ya kuhifadhi
mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata
elimu hiyo ya kilimo.
mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani
Dr Daniel Mafuru Akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo.
Washiriki wakifuatilia.
Post a Comment