Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akitoa
maelekezo kwa watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mara
baada ya kukagua jengo jipya la abiria (Terminal
III) lililopo katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA, Jijini Dar es salaam.
..................................
Serikali imesema
itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Abiria la Tatu la abiria (Terminal
III) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam ili kuboresha huduma za usafiri
wa anga nchini.
Akizungumza mara baada
ya kukagua mradi huo Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi huo
sehemu ya kwanza ilifadhiliwa na Benki ya HSBC ya Uingereza hivyo sehemu ya
pili Serikali itatoa fedha ili
kukamilisha mradi huo.
”Awamu ya kwanza ya
ujenzi huu tulipata mkopo lakini awamu ya pili ya mradi Serikali tumesema
hatutachukua mkopo, tutajenga kwa fedha zetu za ndani sababu tuna uzoefu mkubwa
wa utekezaji wa miradi kwa kutumia fedha za zetu za ndani'' amesema Prof.
Mbarawa.
Aidha, Prof. Mbarawa
ameongeza kuwa imarishaji wa viwanja vya ndege nchini unakwenda sabamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) ambao mpaka sasa tayari lina ndege mbili aina ya Bombadier
Q400.
|
Post a Comment