Aliyekuwa Rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili Equatorial Guinea
Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili nchini Equatorial Guinea, siku moja baada ya kuachia madaraka kwa Adama Barrow, aliyemshinda katika uchaguzi wa urais mwezi Disemba mwaka jana.
Jammeh alisafiri kwa ndege kutoka Banjul hadi Guinea na baadaye kuendelea na safari yake kwenda Equatorial Guinea.
Hapo jana Bwana Jammeh alitangaza kwamba atang'atuka baada kuongozi Gambia kwa miaka 22.
Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili nchini Guinea . Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake nchini Gambia kumshurutisha Bwana Jammeh kukubali Adama Barrow aapishwe.
Yaya Jammeh akiwapungia mkono watu alipokuwa akiabiri ndege Banjul |
Jumuiya hiyo inasema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watasalia nchini humo kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.
Wanajeshi wa nchi za magharibi mwa Afrika wameingia nchini Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal kuhakikisha kuwa raia wa nchi hiyo, wamejiandaa kwa kurejea nyumbani mtu waliyemchangia kuwa rais, Adama Barrow.
Hii ni baada ya mtangulizi wake Yahya Jammeh kuondoka nchini humo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Senegal Mankeur Ndiaye, anasema kuwa haki za bwana Jammeh zitalindwa lakini viongozi wa kanda hawajakubaliana kuhusu msamaha kwa ukiukaji wa haki za binadamu anaodaiwa kuendesha nchini Gambia
Post a Comment