Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kulia) akisamilia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC), Livingstone Lusinde( kulia) walipowalisi
mkoani wa Iringa, kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani
huo.
...........................
Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya
Umeme Vijijini, Unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Awamu
ya kwanza na ya Pili ili kuona thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali
katika mradi huo.
Mwenyekiti wa PAC,
Livingstone Lusinde alisema hayo mkoani Iringa wakati wa ziara ya kukagua
utekelezaji wa mradi wa REA, katika vijiji na Taasisi mbalimbali zilizopitiwa na Mradi huo.
Lusinde alifafanua
kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo baada ya kuona miundombinu
iliyotumika na maendeleo ya wananchi katika maeneo ambayo yamepitiwa na miradi hiyo.
" Tumepita
katika vijiji mbalimbali hapa Iringa ambayo nimepitiwa na REA,tumeona namna
ambavyo mradi huo umetekelezwa na tumeona miundombinu iliyotumika na maendeleo
yake hivyo hatuna budi kusema wazi kuwa tumeridhishwa na utekelezaji wa mradi
huu", Alisema Lusinde.
|
Post a Comment