MO DEWJI Mshindi Tuzo ya AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE PERSON OF THE YEAR 2016
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ametangazwa na Jarida
la African Leadership kuwa mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine
Person of the year 2016 baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro
kilishohusisha watu nane.
MO Dewji ambaye ni Mtanzania anayejihusisha na biashara
kupitia kampuni yake ya MeTL Group na kusaidia jamii kupitia Taasisi ya MO
Dewji ameibuka mshindi kwa kupata asilimia 60.8 ya kura zote zilizopigwa
akifuatiwa na Rais mstaafu wa Ghana, Dramani Mahama ambaye alipata asilimia
30.2.
Wengine waliowania tuzo hiyo ni Strive Masiyiwa, Chris
Kirubi, Akinwumi Adesina, Cyril Ramaphosa, Atiku Abubakar na Aisha Mohammed.
Akizungumza kuhusu MO Dewji, Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa
Jarida la African Leadership, Joe Beasley amemtaja MO Dewji kama mtu ambaye
anaumuhimu mkubwa kutokana na dhamira yake ya kusaidia bara la Afrika kupunguza
tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutoa nafasi nyingi za kazi.
“Dhamira ya Dewji ni kutengeneza ajira jambo ambalo ni kiini
cha tatizo kubwa linalokabili Afrika la ukosefu wa ajira … kupitia biashara
zake amesaidia kupunguza ukosefu wa ajira, kupata utajiri na kutoa ajira kwa
vijana ambao hawana ajira barani [Afrika],” alisema Beasley.
Mohammed Dewji anakuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2016
ambapo kwa mwaka 2015 ilichukuliwa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodluck
Jonathan.
Post a Comment