Kundi la mifugo likiwa ndani ya Pori Tengefu
la Loliondo, karibu kabisa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
................................
Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii inalaani vikali uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya
Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na
kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia
kukausha vyanzo maji yanayokwenda katika
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof. Jumanne Maghembe amesema maelfu ya mifugo kutoka nchi jirani ya Kenya imekuwa ikiingizwa
ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti muda
wa saa 11 jioni,
Amesema katika kukabiliana na changamoto
ya uharibu wa chanzo kikuu cha maji ya Serengeti kwa asilimia 47.2 ya maji
yote, tayari mifugo 1700 imeshakamatwa
Mbali na mifugo hiyo, Waziri Maghembe alisema kuwa maelfu ya
Matrekta ya kutoka nchini Kenya yameletwa kulima katika maeneo yanayopakana na
Serengeti
Aliongeza kuwa hivi karibuni kilimo kimeshamiri ambapo
kipindi cha nyuma wakazi walikuwa
wanalima na ng’ombe (maksai) ila sasa matrekta ya Kenya yanalima na kufungua
mashamba makubwa.
Kufuatia hali hiyo,
Waziri Maghembe ameagiza kuwa raia wa Kenya wenye mifugo Loliondo warudi makwao mara moja, Mkoa na
Wilaya uchukue hatua kuwaondoa mara moja
Pia, Matrekta yote ya
nchi ya Kenya yawe na usajili wa kodi (Tax Clearance) toka TRA au yarudi kwao
mara moja
Aidha, ameagiza kuwa eneo la 1,5002km liwekewe alama
mara moja na uwekaji alama ukamilike ifikapo tarehe 30 Machi, 2017.
Kwa upande wa Utalii, Ameziagiza kampuni
zote za utalii ambazo hazina usajili wa kitaifa zinazofanya biashara kwa
mikataba ya vijiji ziripoti Wizarani ndani ya siku saba, Ikiwa pamoja na
kuonyesha usajili wao, kuonyesha vitalu walivyopewa na Serikali pamoja
kuiridhisha Serikali kama wanalipa kodi.
Awali, akizungumzia kuhusu mgogoro huo
wa Pori Tengefu la Loliondo, Waziri Maghemba alisema anatambua kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anasimamia
mazungumzo ya wadau wote ili kuleta utatuzi wa mgogoro huo.
‘’Nimeambiwa kuwa mwelekeo wa mazungumzo
ni mzuri nahimiza mazungumzo yaendelee, lakini
nimeona nikingoja hadi mazungumzo
hayo yaishe Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti itakuwa haipo.’’ alisisitiza
|
Post a Comment