Waandishi wa Habari wakiuliza maswali mbalimbali
wakati wa Mkutano huo.
.........................
Na Aron Msigwa –NEC, Zanzibar.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi wanaoishi katika kata
19 zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Madiwani
kwa upande Tanzania Bara na
Ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar Januari 22, 2017 wajitokeze kwa wingi
kupiga kura kuwachagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka 3.
Akizungumza na vyombo vya Habari leo mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles kaijage amesema kuwa
maadalizi ya Uchaguzi huo yamekamilika na wananchi wenye sifa za kupiga kura
katika uchaguzi huo wajitokeze kutimiza wajibu wao wa Kikatiba.
Mhe. Kaijage amewapongeza wananchi wanaoishi
katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na wale
wa Kata 19 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi mdogo hapo kesho kwa utulivu waliouonyesha wakati wa kipindi
cha Kampeni za Uchaguzi huo.
Ameeleza
kuwa licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale zilizojitokeza zikiwemo za
ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwa baadhi ya Vyama na wagombea wao, Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ilichukua hatua za kukemea vitendo hivyo ili kuwezesha
Kampeni za Uchaguzi kufanyika kwa Usalama na Amani.
“Licha ya kwamba kutakuwa na ulinzi wa kutosha
katika vituo vya kupigia kura, Ni matumaini ya Tume kuwa hali ya Amani na
Utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa na kama ilivyokuwa katika Chaguzi zilizopita
itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa Utulivu,
Amani na Ustawi wa Taifa letu” Amesema Jaji Kaijage.
Ameeleza kuwa katika uchaguzi huo jumla ya Wapiga Kura 9,280 wa Jimbo la Dimani
Zanzibar wanatarajiwa kupiga kura ili kumchagua Mbunge atakayewaongoza kwa
kipindi cha miaka 3 kupitia vituo 29 vya Kupigia Kura katika Jimbo hilo.
Kwa upande wa Uchaguzi Mdogo
wa Madiwani katika Kata 19 za Tanzania Bara Wapiga Kura 134,705 walioandikishwa
wanatarajia kupiga kura katika vituo 359
ambavyo vilitumika katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“
Naomba nitumie fursa hii kutoa rai kwa wananchi
waliojiandikisha wajitokeze kwenye vituo vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015 ili waweze kupiga kura kuwachagua viongozi mnaowataka bila hofu,
woga, wasiwasi au ushawishi” Amesisitiza.
Kuhusu mchakato mzima upigaji wa kura ikiwemo
taratibu za kuzingatiwa na wananchi kwenye vituo vya kupigia Kura, uhesabuji wa
Kura, ujumlishaji wa Kura na Utangazaji wa matokeo amesema kuwa hatua zote
zitafanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi kwa kuzingatia Sheria.
Amesema kuwa siku ya uchaguzi Januari 22, 2017 vituo
vyote vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na
kufungwa saa 10:00 jioni na kufafanua kuwa iwapo wakati wa kufunga Kituo
watakuwepo Wapiga Kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na
hawajapiga wataruhusiwa Kupiga Kura.
Jaji Semistocles amesisitiza kwamba mtu yeyote
hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa Wapiga Kura baada ya saa kumi (10:00)
jioni muda ulioainishwa kisheria.
Ameeleza kuwa kwa kila mpiga kura katika jimbo
hiloakumbuke kubeba Kadi yake ya Mpiga Kura kwa kuwa Sheria ya Uchaguzi
inaelekeza kuwa ili Mpiga Kura aruhusiwe kupiga kura ni lazima awe na kadi ya
Mpiga Kura.
“ Naomba ieleweke wazi kuwa Fomu Na. 17 sio
mbadala wa Kadi ya Mpiga Kura, Wapiga
Kura ambao wana Kadi ya Mpiga Kura lakini taarifa zao hazimo katika Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura Kituoni, hawataruhusiwa kupiga kura” Amesisitiza Jaji
Kaijage.
Amesema kuwa ni
marufukuna ni kosa la jinai kumkataza mtu kwenda Kupiga Kura akisisitiza
kwamba siku hiyo ya kupiga kura kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye
ulemavu, wanawake wajawazito au wenye watoto wachanga na wazee ambao
hawatatakiwa kupanga mstari.
Jaji Semistocles amefafanua kuwa wakati wote wa
Kupiga Kura na Kuhesabu Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa watakuwepo kwenye
vituo kwa kuwa wajibu wao ni kulinda maslahi ya Vyama vyao vya Siasa na
Wagombea wao.
Hata hivyo
amesema hawatakiwi kuingilia masuala ya utendaji ambayo yamekabidhiwa kwa
Msimamizi wa Kituo.
Amesema Mawakala hao wataruhusiwa kuwepo Vituoni
kwa mujibu wa Sheria na Kanuni na kusisitiza kwamba Wakala asiyekuwa na barua
ya utambulisho kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na ambaye hatakula kiapo cha
kutunza siri hataruhusiwa kuingia katika Kituo cha Kupigia, Kuhesabia na
Kujumlishia Kura.
Katika hatua nyingine Jaji Kaijage amebainisha
kuwa Kurazilizopigwa zitahesabiwa katika
Kituo cha Kupigia Kura mara tu Upigaji Kura utakapokamilika na matokeo husika ya Kituo kujazwa kwenye Fomu za Matokeo Na. 21B
kwa upande wa Ubunge na Fomu Na. 21C kwa
upande wa Udiwani kisha fomu hizo kutiwa
saini na Msimamizi wa Kituo/Msimamizi Msaidizi wa Kituo, Mawakala wa Vyama au
Mgombea aliye Kituoni.
Amesema nakala moja watapewa Mawakala/Mgombea na
nakala nyingine itabandikwa nje ya Kituo cha Kuhesabia kura ambapo Wakala wa
kila Chama cha Siasa na mlinzi wa Kituo watakaokuwa Kituoni wataruhusiwa
kusindikiza msafara wa kupeleka matokeo ya Uchaguzi kwenda kwa Msimamizi wa
Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata kwa upande wa Tanzania Bara na
kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani kwa
upande wa Zanzibar.
Amefafanua kuwa matokeo yote yakishapokelewa na
Msimamizi wa Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Ubunge na Msimamizi Msaidizi wa
Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Udiwani, yatajumlishwa mbele ya Mawakala na
wote wanaoruhusiwa kuingia kwenye vituo vya Kujumlishia Kura.
“ Kama ilivyokuwa wakati wa Kuhesabu Kura, baada
ya Ujumlishaji kukamilika matokeo ya Ubunge ngazi ya Jimbo yatajazwa katika
Fomu Na. 24B na yale ya Diwani katika Kata yatajazwa katika Fomu Na. 24C, Fomu
za Matokeo hayo zitatiwa saini na Msimamizi wa Uchaguzi na Mawakala watakaokuwepo
watapewa nakala za Fomu za Matokeo na Nakala moja itawekwa mahali pa wazi nje
ya Kituo cha Kujumlisha Kura”
Akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni za uchaguzi huo
amesema zitamalizika leo (Januari 21) saa 12 jioni na Vyama, Wagombea na mashabiki
hawataruhusiwa kufanya kampeni za aina yoyote ikiwa ni pamoja na kutumia alama
zozote zinazoashiria Kampeni kama vile bendera na mavazi ya vyama vyao.
Kuhusu uwazi katika uendeshaji wa uchaguzi huo
amefafanua kuwa vyama vyote vya Siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi vinatakiwa kuhakikisha kwamba vinaweka
Mawakala katika vituo vyote vya Kupigia Kura na Kujumlishia Kura ambao
watatimiza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Jaji Kaijage amesisitiza kuwa kwa
kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yaliyokubaliwa na Vyama vyote vya
Siasa, Wapiga Kura wanatakiwa kuondoka Vituoni mara baada ya kupiga kura ili
kuendelea na shughuli zao kwa kuwa Vyama
vya Siasa vyenye wagombea vitakuwa na Mawakala vituoni ambao watalinda maslahi
ya Vyama na Wagombea wao huku watu waliotajwa kwenye Sheria ya Uchaguzi
wakiwemo wagombea, mawakala, Afisa wa Tume, msimamizi wa Uchaguzi na Afisa
Usalamandiyo wanaoruhusiwa kuingia kwenye Vituo vya Kupigia, Kuhesabia na
Kujumlishia Kura.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za
Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe amewaaeleza waandishi wa Habari kuwa kwa
mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kumtangaza Mshindi ngazi ya Ubunge ni
Msimamizi wa Uchaguzi na kwa ngazi ya Udiwani mwenye mamlaka ya kufanya hivyo
ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Amesema kuwa zoezi la Kupiga Kura, Kuhesabu kura
,KujumlishaMatokeo na Kutangaza matokeo litafanywa kwa uwazi na kwa kuzingatia
Sheria na kutoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi wao.
Amesema kuwa wananchi watakaoruhusiwa kupiga kura
ni wale wenye sifa ambao watakuwa na kadi za kupigia kura na ambao majina yao
yameonekana kwenye Daftari la kudumu la kupigia Kura na kusisitiza kwamba
mwananchi ambaye jina lake halitakuwa kwenye Daftari la Kudumu la kupigia kura
hataruhusiwa kupiga kura.
“Utaratibu wa kupiga kura umeelezwa katika Sheria,
Ukisoma kifungu cha 63 kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi A,
kinaeleza wazi mwananchi anapofika kituoni alipopangiwa na Tume anaonyesha kadi
yake ya kupigia kura na kisha jina lake linaitwa kwa sauti na ikiwa amekidhi
sifa anaruhusiwa kupiga kura asipokidhi sifa Msimamizi wa Uchaguzi anayo
Mamlaka ya kumzuia asipige Kura” Amesema.
|
Post a Comment