Bodi ya Filamu Tanzania yawakutanisha Wadau Kuandaa Sera ya Taifa ya Filamu.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Joyce Fissoo akitoa mchango wake mbele ya wajumbe wanaoshiriki kikao kazi
cha maandalizi ya rasimu ya sera ya filamu nchini. Katikati ni rais wa Shirikisho
la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba.
Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu za kitanzania
Chiki Mchoma akiwasilisha hoja kama mdau watasnia ya filamu mbele ya wajumbe wa
kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu nchini. Wengine kwenye picha kuanzia
kuliani Mwnyekiti wa Bodi kuu Sylvester Sengerema, Mwenyekiti wa kikao Vonavyalo
Luvanda, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso na rais washirikisho
la filamu nchini Simon Mwakifwamba.
Wajumbe mbalimbali wanaoshiriki kikao kazi
cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu nchini wakifuatailia kwa makini hoja inayowasilishwa
na mmoja wa wajumbe wa kikao hicho(hayupopichani). Kikao hicho kinafanyika mjini
Bagamoyo kwenye Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBA).
Wasanii na wadau watasnia ya filamu wanaoshiriki
kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu wakifurahia jambo na mwandishi mkongwe
wa riwaya na miswada ya filamu AmriBawji(mwenye baraghashia).Kikao kazi hicho kinafanyika
ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBA).
.............................................
KILIO cha muda mrefu cha wadau wa sekta ya filamu nchini sasa
kinaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu baada ya Bodi ya Filamu Tanzania
kuwakutanisha wadau wake kwa ajili ya maandalizi ya sera mahususi itakayotoa mwongozo
na kuendeleza sekta hiyo nchini.
Sekta ya filamu nchini imekuwa ikisimamiwa na Sera ya Utamaduni
na Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na. 4
ya mwaka 1976 pamoja na kanuni zake.
Kukosekana kwa sera mahususi ya filamu nchini kuliibua changamoto
mbalimbali.
Changamoto hizo ni pamoja
na kuwepo kwa filamu na michezo mingi ya kuigiza inayotayarishwa chini ya viwango,
kutokuwepo kwa mitaji na uwekezaji wa kutosha,sekta ya filamu kutoendeshwa kibiashara,
kukosekana kwa mifumo bora ya usambazaji, kutokuwepo kwa weledi na ubunifu wa kutosha,
uharamia wa kazi za filamu n.k.
Changamoto zilizoainishwa hapo juu zilibainika baada ya Bodi
ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya tafiti kuhusu hali
halisi ya tasnia (situational analysis).
Katika kikao cha kazi cha wadau kilichofanyika tarehe 3
Oktoba, 2016 katika ukumbi wa uwanja wa Taifa, Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa naMichezo Nape Nnauye,aliagiza uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania na wizara
yake kushirikiana pamoja kuhakikisha sera mahususi ya filamu inapataikana mapema
iwezekanavyo.
Sera hiyo mahsusi ya filamu nchini inategemewa kuwa mwarobaini
wa changamoto zinzoikabili sekta hiyo kwa muda mrefu sasa.
Ikumbukwe wadau watasnia
ya filamu nchini wamekuwa wa kilalamika kukosa mapato stahili yanayotokana na kazi
zao, kushindwa kupata mitaji ya kuwawezesha kuwekeza miundombinu ya kisasa kwenye
uzalishaji na mfumo hafifu wa kupambana na uharamia wa kazi zao.
Post a Comment