Mkuu wa Mkoa wa SINGIDA azindua Ufanyaji mazoezi Kimkoa Wilayani Ikungi
Mkuu wa mkoa wa Singida Rehema Nchimbi akiongoza viongozi na wananchi wa mkoa huo katika uzinduzi wa mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu la kufanya mazoezi ili kuondoa maradhi yasiyoambukiza na kujenga mwili.
1 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi katikati akiwa na Mbunge
wa viti maalum Martha Mlata na mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu wakifanya mazoezi ya viungo katika uwanja wa
shule ya Sekondari Ikungi.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akifanya mazoezi
na mbunge wa viti maalum Martha Mlata.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi
katikati akiwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu wakiwa na mshindi wa
kwanza wa mbio za Mumbai Marathon Alphonce Simbu wakifanya mazoezi baada ya
kumpokea.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akicheza muziki baada
ya mazoezi na mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikungi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akionyesha umahiri
wake kwenye mazoezi ya viungo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiruka juu ikiwa ni moja ya
mazoezi huku baadhi ya viongozi akiwemo mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Rehema
Nchimbi na mbunge wa viti maalum Martha Mlata wakimuangalia.
.................................................
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amezindua mazoezi
kimkoa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan la kufanya mazoezi ili kuondoa maradhi yasiyoambukizwa na
kuimarisha afya za wananchi.
Mbali na uzinduzi huo pia amempokea shujaa mwanariadha Alphonce
Simbu ambaye ni mshindi wa kwanza mbio za Mumbai marathon zilizofanyika mapema
mwezi huu huko India.
Akizindua mazoezi hayo leo wilayani Ikungi mkoani humo, Dk.
Nchimbi aempongeza Simbu kwa kuwakilisha vizuri katika riadha nje ya nje
na kuwahamasisha vijana kuchamkia fursa hiyo ya riadha kwa kuwa inalipa.
“Singida ni tajiri wa mambo mengi kikubwa tuamue tu,inawezekana
kabisa Singida kutoa vipaji zaidi kama tukijipanga,vijana tumieni fursa hii
kwani riadha inalipa na inainua uchumi kama ilivyotokea kwa
Simbu,”alisema dokta Nchimbi.
Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu
amemuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa wilaya hiyo imejipanga kuboresha mchezo wa
riadha ili kuibua vipaji zaidi vya vijana na kuendeleza sifa ya wilaya na mkoa
kwa ujumla katika kutoa wanariadha mahiri watakaoiwakilisha Tanzania kama
alivyofanya Simbu.
Ameagiza mazoezi kufanyika jumapili ya pili ya kila mwezi ili
kujenga miili yetu na kumpatia Simbu vifaa vya michezo na ahadi ya shilingo
milioni moja kwa ajili ya kumsaidia kujiandaa na mashindano yajayo
Akitoa shukrani kwa mapokezi Simbu ambaye ni mzaliwa wa kijiji
cha Mampando,kata ya Ntuntu katika wilaya ya Ikungi amesema mapokezi hayo
yamekuwa chachu kwake ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano yajayo.
Akisoma taarifa ya chama cha riadha mkoa katibu wa chama hicho
mwalimu Beno Msanga ameshukuru serikali ya mkoa na wilaya kwa
ushirikiano wanaoutoa kusaidia mchezo wa riadha na kusema kwa sasa
wana kambi ya wachezaji 15 kujiandaa kwenda mashindano ya mbio za nyika
mjini Moshi tarehe 17 february 2017.
Aidha amesema kwa kutambua mchango wa mkuu wa wilaya hiyo
Mtaturu chama cha riadha mkoa kimemteua kuwa mlezi wa Chama hicho mkoa wa Singida.
Post a Comment