Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali( PAC), wakielezwa na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani( katikati) namna ambavyo kifaa maalum
kinachofahamika kama umeme tayari( UMETA) umeme tayari kinavyofanya kazi.
.............................
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (
PAC) imetoa miezi sita kwa Taasisi na
Mashirika yote kulipa madeni ya ankara wanayodaiwa na Shirika la Umeme nchini
(TANESCO) na endapo watashindwa kufanya hivyo watakatiwa huduma hiyo.
Agizo hilo limetolewa mkoani Mbeya na Mwenyekiti
wa Kamati ya PAC , Livingtone Lusinde wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo
wakati wa kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika kutekeleza Miradi
ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati wa Vijijini( REA) kwa
kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Lusinde alisema Tanesco imekuwa ikishindwa
kutimiza majukumu yake kutokana na kukosa fedha za kutosha kujiendesha na hivyo
kuwakosesha wananchi hudumu muhimu ya umeme katika maeneo mbalimbali .
" Tanesco imetapakaa nchi nzima, lakini haiwezi
kutoa huduma bora za uhakika kwa wateja wake katika maeneo yote hayo kutokana
na miundominu mibovu na kutomfikia mteja kwa wakati kwa vile tu hawana fedha",
alisema Lusinde.
Alifafanua kuwa kwa sasa kila Shirika au Taasisi
inatakiwa kulipa ankara ya madeni yake moja kwa moja kutoka hazina, hivyo PAC inaimani kuwa kwa kipindi cha miezi sita
hawatarajii tena kusikia malalamiko ya madeni ya ankara kutoka tanesco dhidi ya
Taasisi na Mashirika.
|
Post a Comment