Rais Mstaafu ALI HASSAN MWINYI awataka Watanzania kulinda Amani na Utulivu
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani singida Miraji Mtaturu akiwa na
Sheikh wa mkoa wa Singida Sheikh Salumu Mahami wakimsindikiza Rais mstaafu wa
awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi kufungua msikiti uliojengwa na
mbunge mstaafu wa jimbo la Singida magharibi Khalifa Mohamedi Missanga
mwenye koti jekundu nyumbani kwake kijiji cha Mnang'ana kata
ya Sepuka wilaya Ikungi, ufunguzi huo umefanyika jana kabla ya
swalatil Jumaa.
Waumini mbalimbali waliohudhuria ufunguzi huo
wakimsikiliza mgeni Rasmi Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Ali Hassan
Mwinyi kwenye viwanja vya msikiti wa Ititi, Sepuka wilayani Ikungi mkoani Singida.
.............................
Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi
ametoa rai kwa watanzania kulinda amani na utulivu iliyopo nchini ambayo ni
tunu ya Taifa na uhai wa watanzania.
Mzee Mwinyi ametoa rai hiyo wilayani Ikungi mkoani Singida wakati
akifungua msikiti uliojengwa na mbunge mstaafu wa jimbo la Singida magharibi
Khalifa Mohamedi Missanga kijiji kwake Mnang'ana kata ya Sepuka
wilaya humo.
Katika salam zake Mzee Mwinyi amewaasa waislam nchini
kupendana na kuvumiliana na kusisitiza kila mmoja kushika kile
anachoamini.
"Ndugu zangu nawaasa tupendane, tuvumiliane,hata kama kuna
hitilafu za kimadhehebu zisiwakosanishe,"alisema.
Rais huyo mstaafu aliongeza " hitilafu zipo tu kikubwa ni
kushika kile unachoamini na ukitaka kumlingania mwenzako basi iwe kwa lugha
laini na yenye heshima lakini kikubwa tulinde amani kwani ndio uhai wetu,"
Msikiti huo uliofunguliwa ulianza kujengwa mwaka 2012 na
umekamilika kwa thamani ya milioni 58.
Post a Comment