Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, alipokuwa akifunga semina ya mawakala hao, leo Janauari 20, 2017. Uchaguzi mdogo wa Unatarajiwa kufanyika Jumapili hii nchini kote.
--------------
Na Bashir Nkoromo
Akifunga semina hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliwashangaa wapinzani kwamba kwa nini kila baada ya uchaguzi huwa wanalalamika kuwa wameibiwa kura.
"Zamani wakati mimi ni Mbunge, wakati wa uchaguzi, kura zilikuwa zinaenda kuhesabiwa wilayani, lakini siku hizi Mawakala wa vyama vyote wapo, walinzi wapo, tena kura zikishapigwa zinahesabiwa hapohapo kisha matokeo yanabandikwa ukutano hapohapo, wizi huo wa kura utatokea wapi?" alisema na kuhoji Kinana.
Kinana aliwaasa mawakala wa CCM katika uchaguzi huo mdogo wa Kijichi, kuhakikisha kila mmoja anatimiza waibu wake na kusema kwamba, anao uhakika ikiwa mawakala hao watafanya kazi zao vizuri basi CCM itashida.
"Ndugu zanguni, uchaguzi unazo sehemu nyingi, kuna kuteua wagombea, kupiga kampeni, na kupiga kura. sasa katika hatua zote hatua iliyokubwa zaidi ni hii ya kupiga kura, maana hapa ukiharibu umekosa kila kitu", alisema Kinana.
Alisema, japokuwa uchaguzi wa Udiwani katika kata hiyo ya Kijichi ni uchaguzi mdogo, lakini ni lazima kusimama kidete na kuhakikisha CCM nashinda tena kwa kishindo.
"Kweli huu ni uchaguzi mdogo, lakini nachotaka kuwaambia ni kwamba, uchaguzi ni kama kufanyiwa upasuaji, kama unafanyiwa upasuaji wataalam wanaweza kuuita mdogo, lakini wewe unayeenda kupasuliwa usiseme hivyo, ni kama vile kesi inayokukabili mahakamani, unaweza kuidharau ukatahamaki umefungwa, basi tusidharau kamwe uchaguzi huu", alisema, Kinana.
|
Post a Comment