Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta
(PURA) na Wizara ya Nishati na Madini wakijadiliana jambo kabla ya kukutana na
kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mjini Dodoma.
...................................
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi
Kapuulya Musomba ameileza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa, hivi
sasa zaidi ya asilimia 50 ya umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unatokana na
gesi asilia.
Mhandisi
Musomba aliyasema hayo hivi karibuni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha Taarifa
ya Utekelezaji wa Miradi ya TPDC kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba, 2016
na kuongeza kuwa, mipango ya Serikali ni kulifanya Shirika hilo kuchangia zaidi
mapato Serikalini yanayotokana na rasilimali hiyo.
Aidha,
alieleza kuwa, kwa kuwa Tanzania imeingia kwenye uchumi wa Gesi asilia, shirika
linajipanga kuwekeza kwenye shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji na
usambazaji wa gesi ili Taifa linufaike na rasilimali hiyo.
Akifafanua
shughuli ya usambazaji gesi asilia kwa kuzalisha umeme, alisema kuwa, TPDC
inaendelea kuhakikisha kwamba mitambo ya kuzalisha umeme inaunganishwa na
miundombinu ya usambazaji gesi asilia ili iweze kutumia gesi asilia kuzalisha
umeme.
“Mheshimiwa
Mwenyekiti, TPDC kwa kushirikiana na TANESCO iliendelea kusimamia ujenzi wa
miundombinu ya Kudumu ya usambazaji gesi asilia kwenye mitambo ya Kinyerezi I,
Ubungo II,Tegeta na IPTL,”alisema Musomba.
|
Post a Comment